Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy ameshikiliwa na vyombo vya usalama vya nchi hiyo akituhumiwa kupokea rushwa kutoka kwa rais wa zamani wa Libya, Moammar Gaddafi kuchangia kampeni ya uchaguzi wa mwaka 2007.
Sarkozy anatuhumiwa kupokea kiasi kikubwa cha fedha kilichotumwa kupitia masanduku kadhaa, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.
Jana, mwanasheria huyo alihojiwa na maafisa wa usalama pamoja na wataalam wa masuala ya rushwa kwa tuhuma za kupokea rushwa, utakatishaji fedha na kukwepa kodi.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Brice Hrtefeux ambaye alikuwa mmoja ya mawaziri wa Serikali ya Sarkozy, alihojiwa pia kama sehemu ya wahusika.
Sakata hilo ni kubwa zaidi kuwahi kutokea tangu Sarkozy alipokoma kuwa rais wa nchi hiyo mwaka 2012.
- Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Machi 21, 2018
- Diamond aeleza bifu yake na Ali Kiba ilivyosukwa ‘kumuua’
Mwaka 2011, wakati majeshi ya NATO yakimuondoa Gaddafi madarakani, mtoto wake, Seif al-Islam aliviambia vyombo vya habari, “Sarkozy lazima arudishe kwanza pesa alizochukua Libya kwa ajili ya kumsaidia katika kampeni za uchaguzi.”