Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametoa zawadi ya magari na nyumba kwa wanamichezo wa nchi hiyo walioshinda medali katika michuano ya Olimpiki iliyofanyika mjini Tokyo, Japan.

Uganda walipeleka wanamichezo 25 kwenye michuano hiyo, na kufanikiwa kushinda medali nne, mbili za dhahabu, moja ya fedha na moja ya shaba.

Joshua Cheptegei aliyeshinda medali ya fedha katika mbio za mita 10000 na kushinda dhahabu katika mbio za mita 5000 alipewa Mitsubishi Pajero Sport.

Magari ya zawadi kwa washindi.

Peruth Chemutai aliyeshinda medali ya dhahabu katika steeplechase mita 3000 Parejo Sport ya bluu na Jacob Kiplimo aliyeshika nafasi ya tatu na kushinda medali ya shaba kwenye mbio za mita 10000 amepewa
Pajero Sportero L200 ya kijivu.

Baada ya kukabidhi zawadi za magari, Rais Museveni akaahidi kuwajengea nyumba wazazi wa washindi wa medali za dhahabu.

Pia washindi hao watakuwa wakilipwa mshahara kwa mwezi.
Washindi wa medali za dhahabu watalipwa USD 1420 kwa mwezi (Tsh milioni 3), washindi wa medali za fedha watalipwa USD 851 (Tsh Milioni 1.9) na USD 283 (Tsh Laki 6) kwa washindi wa medali za shaba.

Tanzania yaalikwa michuano ya COSAFA 2021
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Augusti 13, 2021