Mahakama ya Katiba Nchini Uganda imeidhinisha mageuzi ya katiba ambayo yameondoa kikomo cha umri wa kugombea kiti cha urais.
Majaji wanne kati ya watano wa jopo la majaji wamesema kuwa mageuzi hayo hayakiuki katiba, na pia hayendi kinyume na muongozo wa bunge nchini humo.
Hii ina maana kwamba Rais wa nchi hiyo Yoweri Kaguta Museveni atakua huru kugombea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2021 ambapo atakuwa amevuka umri wa awali ambapo mwisho wa kugombea ilikuwa ni miaka 75.
Aidha, kikao cha kutoa uamuzi huo uliowasilishwa katika mahakama kuu huko Mbale nchini humo kilianza kwa naibu jaji mkuu, Alfonse Owiny-Dollo, kuanza kwa kuomba radhi kwa mahakama kuchelewa kuanza kwa muda uliopangwa awali.
Hata hivyo, mahakama imekataa kuongeza miaka ya wabunge waliotaka kubaki madarakani kwa miaka 7 badala ya mitano ya sasa.
-
Mkuu wa Majeshi Iran amvaa Trump, ‘anzisha tumalize’
-
Korea Kaskazini yarejesha mabaki ya Wamarekani waliokufa vitani
-
Mtu mzee zaidi duniani afariki, vyakula vyake vyatajwa