Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi, amesema ataendelea kujitahidi kutimiza ahadi alizowaahidi wananchi wa Zanzibar na kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha 2020/2025.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo wakati alipokutana na Wenyeviti wa Chama cha Mapinduzi Mikoa ya Tanzania bara na Zanzibar, waliofika Ikulu Zanzibar kufuatia mwaliko wa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan wa kuhudhuria Tamasha la Kizimkazi 2023.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi.

Naye Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa , Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora, Mzee Hassan Wakasuvi akizungumza kwa niaba ya Wenyeviti wa CCM wa Mikoa amempongeza Rais Dkt. Mwinyi kwa mabadiliko ya maendeleo yaliyofanyika Zanzibar.

Amesema, chini ya uongozi wake aendelee kutekeleza vema ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025 na kutimiza ahadi na kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar na kumtia moyo kuwa viongozi walioko Tanzania bara wamejionea mabadiliko yaliyofanyika Zanzibar.

Gamondi: Kila mchezaji atafunga Young Africans
Siri ya Kocha kutimuliwa yafichuka Singida FG