Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa corona ambayo inatarajiwa kutolewa nchini ni hiari na hakuna mtu atakayelazimishwa kufanya hivyo kwa nguvu.
 
Dk. Mwinyi amesema hayo akiwa katika Ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM), Mahonda Mkoa wa kaskazini Unguja wakati akizungumza na viongozi wa CCM wa mkoani humo katika ziara ya kuwashukuru wananchi na wanaCCM wa Mkoa huo baada ya kukichagua chama  hicho kushika hatamu ya kuongoza dola katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana.

Amesema kuwa Serikali italeta chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa Corona lakini hiyo itakuwa hiari kwa mtu anayehitaji na si lazima kama baadhi ya wananchi wanavyodai kiasi cha kuzusha taharuki.
 
Mwinyi amesema chanjo hiyo itatolewa kwa mahujaji wanaotarajiwa kufanya ibada ya Hijja huko Makka, Saudi Arabia ambayo ni sehemu ya masharti ya Serikali hiyo kwa mahujaji watakaotekeleza ibada ya Hijja ili kupunguza uwezekano wa kuibuka kwa mlipuko wa maradhi hayo.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Mei 30, 2021
Billion 17 kutumika ujenzi wa chuo cha ufundi Dodoma