Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wasanii wa Muziki wa Bongo Fleva walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu, wakiwa Zanzibar baada ya kushiriki katika Tamasha la Muziki la Nandy lililofanyika julai 21, 2021 katika Uwanja wa Mao Zeding.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Wasanii wa Muziki wa Bongo Fleva walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva Faustina Charles ( Nandy ) akizungumza wakati walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, akiwa Zanzibar katika onesho lake la Tamasha la Muziki la Nandy lililofanyika jana usiku 21-7-2021 katika Uwanja wa Mao Zedung Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Wasanii wa Muziki wa Bongo Fleva ukiongozwa na Mwanamuzi Nandy, walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, wakiwa Zanzibar katika Tamasha la Muziki la Nandy lililofanyika jana usiku 21/7/2021. Katika uwanja wa Mao Zedung Jijini Zanzibar.