Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiambatana na Mama Mariam Mwinyi ametoa sadaka kwa watu wenye mahitaji maalumu.

Mahitaji hayo, yametolwa kwa Wazee, Yatima, Wajane na wasiojiweza Wilaya ya Micheweni na Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba hii leo Aprili 12, 2023.

Mara baada ya kutoa msaada huo, Rais Dkt. Mwinyi amewahimiza watu wenye uwezo kuendelea kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu, hasa katika Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani.



