Rais wa klabu bingwa nchini Ufaransa Paris Saint-Germain (PSG) Nasser Al-Khelaifi na katibu mkuu wa zamani wa FIFA Jerome Valcke watasomewa hukumu ya kujihusisha na rushwa mnamo Septemba 2020.
Wawili hao wanakabiliwa na kesi hiyo inayoendeshwa na mahakama ya Uswizi kufuatia tuhuma zinazowakabili za haki za utangazaji.
Taarifa iliyotolewa na mahakama hiyo jana Jumanne, tayari ushahidi umeshakamilika na mwezi Septemba, hukumu itatangazwa kwa wadau hao wa soka.
Al-Khelaifi na Valcke watahukumiwa katika mji wa mashariki mwa Uswizi wa Bellinzona pamoja na mtu wa tatu, ambaye hajatajwa kwa jina moja, kwa utapeli mbaya wa jinai, uchochezi wa utapeli wa jinai, hati za uwongo na ufisadi, imeeleza taarifa hiyo ya mahakama ya uhalifu.
Al-Khelaifi, ambaye pia ni bosi wa kituo cha runinga cha Qatari BeIN Sports, anatuhumiwa kutoa zawadi zisizofaa (hongo) kwa Valcke ili kupata haki za utangazaji za matukio makubwa (ya kifahari), pamoja na Kombe la Dunia la mwaka 2026 na 2030.
Tayari katibu mkuu wa zamani wa FIFA Jorome Valke amefungiwa kutojihusisha na masuala ya soka na kwa miaka 12. Kiongozi huyo chini ya utawala wa rais wa FIFA aliyepita Sepp Blatter alihukumiwa kifungo hicho kwa tuhuma za ufusadi.