Rais wa Urusi, Vladimir Putin amesema kuwa yuko tayari kukutana na Rais wa Marekani, Donald Trump ili kuweza kutafuta ufumbuzi wa mgogoro unaofukuta baina ya nchi hizo.
Wakati huo huo balozi wa Urusi nchini Australia amesema kuwa dunia inaweza kuingia katika hali ya vita baridi ikiwa mataifa ya magharibi yataendeleza chuki dhidi ya Moscow.
Aidha, kwa mujibu wa Msemaji wa Ikulu ya Urusi (Kremlin) Dmitry Peskov, amesema kuwa Putin yuko tayari na Urusi yenyewe iko tayari kuendeleza mahusiano ya pande mbili kwa kulingana na uaminifu wa kila nchi, ikiwemo Marekani.
Hata hivyo, Marekani na zaidi ya mataifa mengine 20 yalitangaza wiki hii kwamba yanawafukuza Wanadiplomasia wa Urusi katika kile kinachoonekana ni kushikamana na Uingereza, katikati mzozo baina ya mahasimu hao wa zamani wa vita baridi.