Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametoa wito kwa Nchi za Ulaya na Marekani kuondoa vikwazo vya safari kwa Mataifa ya Kusini mwa Afrika yaliyobainika kuwa na aina mpya ya Virusi vya Corona
Rais Ramaphosa amesema kugundulika kwa aina ya kirusi cha Omicroni kunatokana na ufanisi na juhudi za Wataalamu wa Afya Nchini Afrika Kusini.
Ameongeza Marufuku ya Usafiri kwa Mataifa ya Kusini mwa Afrika haina uhalali wowote na inaongeza ubaguzi kwa nchi za Kusini mwa Afrika na haisaidii kuzuia madhara ya maambukizi bali inaongeza maumivu ya Kiuchumi.
Uingereza, EU na Marekani ni miongoni mwa walioweka marufuku ya kusafiri.