Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuunda Kamati nyingine Huru itakayo chunguza Mauaji yaliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Mtwara na kuleta taarifa.

Akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Magu alipokuwa njiani kuelekea Mkoani Mara kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Rais samia amesema haiwezekani mauaji yafanywe na Jeshi la Polisi alafu jeshi lijichunguze lenyewe.

“Taarifa niliyonayo Sasa Jeshi limetengeneza kama to ya kufanya uchunguzi alafu walete taarifa haiwezekani Jeshi lifanye mauaji Jeshi lichunguze lenyewe,” Amesema Raise Samia.

Amesema kuwa kamati huru ilete ripoti na kulinganisha ripoti ya polisi nakuona taarifa zinasemaje na kuchukua hatua muafaka.

Aidha Rais Samia ameliagiza Jeshi la Polisi kujitafakari ili kuona kinachotokea.

Diego Costa asaka timu Ulaya
TACAIDS yateta na waandishi wa Habari