Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu ameitaka Wizara ya Habari kuwafungulia Vyombo vya Habari vilivyofungiwa huku akisisitiza wafuate Sheria.

Rais Samia ametoa agizo hilo Ikulu, jijini Dar es Salaam leo April 6, 2021 akizungumza mara baada ya uapisho wa viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni.

Pia, ametaka Kanuni ziweke wazi makosa na adhabu zake ili kusiwe na ubabe kwa kuwa Serikali inaamini katika Uhuru wa Vyombo vya Habari.

Aidha, ametaka Wasanii waangaliwe kwa umakini ili kukuza vipaji vinavyoibuka kila siku pamoja na kutunza tamaduni na silika ya Tanzania japo hatuna tamaduni moja.

Young Africans yabadili 'GIA' angani
Al Merrikh wavamia Kinshasa