Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewabadilisha vituo wakuu wa Mikoa Wawili (Arusha na Simiyu) mara baada ya kuwaapisha pamoja na wenzao.

Amemuhamishia David Kafulila Mkoa wa Simiyu badala ya Arusha ambapo alimpangia awali na kumpeleka John Mongela Arusha ambaye awali alipangiwa Simiyu.

Akizungumza mara baada ya kuwaapisha wakuu wa mikoa na watendaji wakuu wa taasisi leo Mei 19, 2021 ikulu Jijini Dar es Salaam Rais Samia ameeleza sababu za kufanya hivyo ni kutokana na uzoefu alionao Mongella katika ngazi hiyo na ndio maana kamuamishia Jijini Arusha.

“Nimefanya mabadiliko kwa wakuu wa mikoa wawili, mheshimiwa Kafulila aliyekuwa amepangwa Arusha na Mongela ambaye alikuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu; Mongela kwa sababu ulikuwa unaongoza mkoa mkubwa ambao ulikuwa jiji na unaendelea kuwa jiji, utakwenda Arusha na Kafulila kwa sababu ndiyo anaanza kuwa mkuu wa mkoa alikuwa RAS yeye atakwenda Simiyu,” amesema Rais Samia.

Sambamba na hayo yote Rais Samia amewataka walioapishwa wawe na wajibu katika utendaji kazi wao wa kazi katika maendeleo ya nchi.

Kocha Hunt aihofia Simba SC kwa Mkapa
Sakata la LUKU laondoka na meneja