Rais Samia afanya mazungumzo na mtendaji wa sera za maendeleo WB
3 years ago
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemshukuru Mkurugenzi wa Mtendaji wa sera za Maendeleo na Ubia wa Benki ya Dunia, Profesa Mari Pangestu, baada ya kukutana leo Novemba 15, 2021 na kufanya mazungumzo ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia fedha zinazotolewa na Benki hiyo.