Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi tofauti tatu.

Amemteua Prof Ulingeta Mbamba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade). Prof. Mbamba anachukua nafasi ya Dk. Ng’wanza Kamata Soko aliyemaliza muda wake.

Pia amemteua Zuhura Sinre Muro kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano (TTCL). Muro ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ushauri Elekezi ya Kazi Service Limited na Mkufunzi wa muda katika Taasisi ya Uongozi Institute, Jijini Dar es Salaam

Vilevile amemteua Prof. Leonard James Mselle kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Tahema. Prof Mselle ni Mhadhiri, Rasi Ndaki ya Sayansi za Kompyuta na Elimu Angavu, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Juma Duni Haji ashinda uenyekiti ACT Wazalendo
Watoa huduma wa utalii kujengewa uwezo