Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Makame Mbalawa, Mkurugenzi wa TPA na Mkurugenzi Taasisis ya Kupambana na Rushwa TAKUKURU kupitia upya ripoti ya mfumo wa Enterprises Resource Planning ERP unaotumika ndani ya bandari ili kubaini madudu yanayoendelea.
Akizungumza kati hafla ya uzinduzi wa marekebisho ya ghati 0 mpka ghati namba 7 Rais Samia amesema kuwa taarifa ya ukaguzi maalumu ya kiuchunguzi wa mfumo wa ERP umeonyesha kiasi cha fedha nyingi kimetumika kuajiri makampuni mbalimbali ya kuanzisha mifumo ya kieletroniki ya ukusanyaji mapato ambayo haikutoa tija iliyokusudiwa .
Amesema kuwa mifumo haiko vizuri wafanyakazi wanachezea mifumo, wanadanganya na mifumo ambayo haisomi.
Nimesema mifumo hii inatetereka karibuni hapa nilipata taarifa kwamba wafanyakazi wanachezea mifumo ile hasa wa sehemu za hesabu kiasi ambacho ukisoma mfumo unaonyesha mizigo inayoshushwa imelipwa na magetini wanasoma mizigo imelipiwa ukweli ni kwamba mizigo haijalipiwa,” Amesema Rais Samia.