Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Tanzania na Zambia zinajipanga kuhakikisha Reli ya TAZARA inafanya kazi kwa uwezo wake wote na kuchochea uchumi wa nchi hizo mbili.
Akihutubia kwenye Bunge la Zambia jioni ya Oktoba 25, 2023, Rais Samia amesema kwasasa Reli hiyo inafanya kazi kwa asilimia nne tu ya uwezo wake jambo linalohitaji mabadiliko.
Reli ya TAZARA ina uwezo wa kusafirisha kiasi cha tani za mizigo Milioni Tano, lakini kwasasa kiasi cha tani 184,000 pekee, ndizo zinazosafirishwa.
Aidha, Rais Samia Suluhu Hassan (Tanzania) na Rais Hakainde Hichilema (Zambia), waliazimia kuweka mazingira yatakayofanya Biashara kati ya Mataifa haya mawili zisiwe na vikwazo.