Rais Samia Suluhu Hassan, ameipongeza Klabu ya Simba SC, baada ya kufanikiwa kushinda mchezo wa Mkondo wa Pili wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, na kutinga Hatua ya Makundi ya michuano hiyo.

Simba ilitinga hatua hiyo jana Jumapili (Oktoba 16), katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam, kwa kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya CD Primeiro de Agosto ya Angola.

Ushindi huo umeifanya Simba SC kupata ushindi wa jumla wa 4-1, wakitangulia kushinda ugenini Luanda-Angola kwa 1-3, kabla ya kushinda nyumbani Dar es salaam 1-0.

Kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Kimajii wa Instagram ambao upo varrified, Rais Samia aliposti picha ya kikosi cha Simba na kusindikiza na ujumbe wake wa pongezi.

“Kongole @SimbaSCTanzania kwa ushindi wa 1-0 (ushindi wa jumla 4-1) mlioupata dhidi ya timu ya Primeiro De Agosto ya Angola na hivyo kufanikiwa kuingia hatua ya makundi ya klabu bingwa Barani Afrika. Nawatakia kila kheri katika michuano inayofuata.”

Bao la ushindi la Simba SC kwenye mchezo wa jana Jumapili (Oktoba 16) lilifungwa na Mshambuliaji kutoka Zambia Moses Phiri, ambaye pia alifunga kwenye mchezo wa Mkondo wa Kwanza uliopigwa Luanda-Angola.

Mabao mengine ya ugenini yalifungwa na Kiungo kutoka Zambia Clatous Chotta Chama pamoja na Beki wa kulia kutoka Tanzania Israel Patrick Mwenda.

Mo Dewji: Tutafanya mabadiliko, hakuna kurudi nyuma
Rais Samia azima Jenereta, awasha umeme wa Tanesco