Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania itatenga eneo la ekari 20 katika mkoa wa Pwani kwa ajili ya kuhudumia mizigo kutoka Zambia.
Rais Dkt. Samia ameyasema hayo wakati akitoa hotuba kwenye maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Zambia ambapo alikuwa ni mgeni rasmi.
Amesema, “Zambia ni mteja mkubwa wa bandari ya Dar es Salaam, ikichukua asilimia 34 ya mizigo yote inayopitia Bandari hiyo kwenda nje ya Tanzania.”
Aidha, Rais Samia pia ametumia fursa hiyo kusema kwamba mipaka ya kijiografia baina ya Tanzania na Zambia haipaswi kuwa kikwazo cha biashara na uwekezaji baina ya nchi jirani.