Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasihi watumishi wa serikali na sekta binafsi kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha wanapata kipato halali na kujiepusha na vitendo vya wizi, rushwa, ubadhirifu na urasimu.

Ameyasema hayo wakati akihutubia na kutoa salamu za Eid El Fitr kwenye Baraza la Eid leo Mei 14, 2021 kwenye viwanja vya Karimjee na kuwasihi Waislamu kuendelea kumcha Mungu na kutenda matendo mema hata baada ya kumaliza Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kupitia hotuba yake kwenye Baraza hilo Rais Samia amewahimiza wafanyabiashara wote nchini kulipa kodi stahiki kwa serikali na sio kukwepa kwani kufanya hivyo kutaifanya serikali ishindwe kutoa huduma muhimu kwa wananchi.

Aidha, Rais Samia amewapongeza waislamu wote nchini kwa kumaliza mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambayo ni nguzo ya nne katika nguzo tano za dini ya kiislamu.

Sambamba na hayo, Rais Samia amewapongeza Waislamu wote na kuwashukuru waumini wa dini nyingine kwa kushirikiana na kwa namna moja au nyingine katika kipindi chote cha Ramadhani, akisema hiyo ndiyo sifa ya Tanzania na kuhimiza kuendeleza utamaduni huo ulio enziwa na waasisi wa Tanzania.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Mei 15, 2021
Mahakama ya Juu yazuia pendekezo la kubadilisha katiba