Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na mijadala inayoendelea bungeni ya kumlinganisha na mtangulizi wake, Hayati Dkt. John Magufuli.

Akizungumza katika kongamano la viongozi wa dini jijini Dodoma, Rais Samia ameonekana kukerwa na mjadala unaoendelea miongoni mwa Wabunge wa chama kinachoongoza dola (CCM), ambao wamegawanyika katika makundi mawili, kundi moja likitetea rekodi ya Rais aliyepita John Magufuli na linigine linalokosoa baadhi ya mambo ya utawala huo.

Rais Samia amesema yeye na Magufuli ni kitu kimoja na anaendeleza kazi iliyofanywa na mtangulizi wake huyo aliyefariki dunia Machi 17, 2021 kwa ugonjwa wa moyo.

”Inasikitisha sana kuona kwamba watu wanapiga ngoma mitandaoni, lakini ngoma ile inachezwa bungeni, kwa kulinganisha watu na sio kulinganisha ajenda za kitaifa, ajenda ya kitaifa ni moja, mnalinganisha Magufuli na Samia hawa watu ni kitu kimoja,” amesema Rais Samia.

”Awamu ya sita haikutokana na uchaguzi, haikutokana na chama kingine cha siasa, imetoka ndani ya chama cha Mapinduzi, imetokana na uongozi uliokuwepo wa awamu ya tano,” amesema Rais Samia.

Gomes: Young Africans wasahau kuhusu ubingwa.
Wezi wavamia kanisa, wapora nguo za ndani

Comments

comments