Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Tundu Lissu, ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jijini Brussels nchini Ubelgiji.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Rais Samia na Lissu wamezungumzia masuala mbalimbali yenye maslahi ya ustawi wa Tanzania.
“Mazungumzo hayo yamefanyika baada ya Rais Samia kukubali maombi ya kiongozi huyo wa Chadema kukutana naye na kuzungumza jijini Brussels,” imeeleza taarifa hiyo.
Rais Samia yuko nchini Ubelgiji ambapo ameingia leo akitokea nchini Ufaransa alikokohudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa.
Mwaka jana, Lissu aliweka wazi kuwa alitafuta nafasi ya kuzungumza na Rais Samia kwa njia ya simu, lakini hakufanikiwa kutokana na ratiba ya kiongozi huyo.