Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekutana na Malkia wa Uholanzi Maxima ambaye pia ni Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN, katika masuala ya Mfumo Jumuishi wa Fedha katika Maendeleo na kuzungumza na Wanahabari, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais Samia, amekutana na Malkia huyo hii leo Oktoba 19, 2022 ambaye anahitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu iliyoanza Oktoba 17, 2022 baada ya kuwasili Jijini Dar es Salaam, akitokea mkoani Kilimanjaro hapo jana Oktoba 18, 2022.
Kabla ya kuhitimisha ziara yake hapa nchini, Mlkia Maxima pia alikutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali, akiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Robert Kahendaguza.
Rais Samia anakutana na kiongozi huyo akitokea Mkoani Kigoma, ambapo alitembelea na kuzindua miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo kuandika historia kwa Mkoa huo kupata umeme wa Tanesco toka Gridi ya Taifa ambao haikuwahi kuupata tangu kuzaliwa kwa Taifa la Tanzania.