Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amekutana na Mwenyekiti na Rais wa Big Win Philanthropy Jamie Cooper aliyeambatana na Ujumbe wake, Waziri wa TAMISEMI Innocent Bashungwa pamoja na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe Dodoma leo tarehe 26 Machi, 2022.

Kikao hicho kina lengo la kuangalia fursa za Uwekezaji kwenye Mamlaka za Serikali za
Mitaa zenye lengo la kuinua maisha ya watanzania.

Ujumbe toka Ofisi ya Rais – TAMISEMI umeongozwa na Waziri Innocent Bashungwa, Katibu Mkuu Prof. Riziki Shemdoe na wataalam toka idara mbalimbali

Katika kikao hicho kwa pamoja wamekubaliana kuanza na fursa zilizopo katika eneo la Kilimo ambalo linaajiri Vijana wengi pamoja na Wanawake kwa kuboresha uzalishaji, mnyororo wa thamani na masoko.

Wataalam wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, na Wizara ya Kilimo wanaendelea na kuandaa maandiko yatakayowezesha kuanza kwa utekelezaji wa maazimio ya kikao hicho.

Lengo la Ujumbe wa Big Win Philantrophy ni kusaidia katika kuibua fursa za uwekezaji kwenye jamii na kuhakikisha kuwa zinaleta manufaa kwenye hamii husika.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mwenyekiti na Rais wa Big Win Philanthropy Jamie Cooper mara baada ya kikao chao kilichofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 26 Machi, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha na Mwenyekiti na Rais wa Big Win Philanthropy Bi. Jamie Cooper aliyeambatana na Ujumbe wake Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 26 Machi, 2022.

Makamu wa Rais Dkt Mpango atoa maagizo JKT makutupora
Bashungwa awataka mameya kutangaza fursa za uwekezaji