Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameeleza kuridhishwa na utendaji kazi wa Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko katika kuisimamia Sekta ya Madini.

Rais Samia, ameyasema hayo hii leo Oktoba 16, 2022 wakati akiwasalimu wananchi wa Runzewe Jimbo la Bukombe mkoani Geita na kuzungumza nao masuala mbalimbali akiwa safarini kuelekea mkoani Kigoma.

Amesema, “Ndio maana mnaona nawagusa wote nawabadilisha lakini Biteko yupo hapo katika Wizara ya Madini kwa sababu ninaye kijana anayefanya kazi nzuri na anaisaidia Tanzania.”

Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko.

Aidha Rais Samia ameongeza kuwa, mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 4 na sasa unachangia karibu asilimia 8 ya mchango wake kwa Taifa.

Amemtaka Waziri Biteko, kuhakikisha mchango wa Sekta ya Madini unafikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2025 ili iweze kuchangia zaidi katika Pato la Taifa.

Hata hivyo, amemtaka kuongeza bidii katika kusimamia shughuli za kuisimamia Sekta kwa kuwa anao uwezo wa kutosha katika shughuli za madini.

Siku ya Chakula Duniani: Vifo vya njaa jambo la kawaida
Gesi chanzo ajali ya mgodini, vifo vyafikia 41