Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko, kupisha uchunguzi.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Machi 28, 2021 baada ya kupokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na Takukuru Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma.

“Ripoti nimeiona, nimeipitia na nimebaini ubadhirifu mkubwa uliofanywa pale bandari, nakuomba Takukuru jishughulishe pale, alipita Waziri Mkuu alilishughulikia”.

“Waziri Mkuu aliunda kamati na wakafanya uchunguzi kidogo ambao yaliyotoka, hatua chache zilichukuliwa lakini imani yangu ni kwamba kama kuna ubadhirifu pale waliosimamishwa ni hawa wa chini huku, ninaomba mara moja nitoe agizo la kumsimamisha Mkurugenzi Mkuu wa Bandari halafu hatua zaidi ziendelee,” amesema Rais Samia.

Mahakama: Rais amlipe fidia mwandishi aliyemdhalilisha
Zanzibar wafanya Uchaguzi mdogo jimbo la Pandani