Katika mtandao maarufu Duniani wa Google nchini India, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekua mtu wa pili kwa habari zake kutafutwa sana nchini India kuliko jambo lingine lolote.
Ikumbukwe India ni Taifa lenye idadi ya watu bilioni moja na milioni mia tatu (sawa na takribani mara 21 ya idadi ya Watanzania wote), ikiwa nimiongoni mwa nchi vinara kwa matumizi ya mtandao.
Jana raia wa India na mshindi wa Tuzo ya Nobel, Amartya Sen alifariki dunia lakini alizidiwa kwa kuangaliwa mitandaoni na Rais Samia, huku Nyota wa zamani wa Real Madrid na Chelsea, Eden Hazard ambaye jana alitangaza kustaafu soka, akishika namba nne.
Nafasi ya kwanza ilishikwa na nyota wa mchezo wa Kriketi wa Pakistan, Babar Azam ambaye alicheza vibaya kiasi cha kutolewa kwenye mechi dhidi ya Pakistan na ikumbukwe Kriketi ndiyo mchezo unaopendwa zaidi nchini India, huku nafasi ya pili ikishikwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.