Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan yupo katika uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi, akiongoza kilele cha maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani kinachofanyika hii leo Desemba mosi, 2022.
Maadhimisho hayo yenye kaulimbiu “Imarisha Usawa” pia yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na mashirika akiwemo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye.
Hata hivyo, takwimu zinaonesha kuwa vijana wengi ndio wanaongoza kwa kupata maambukizi zaidi ikilinganishwa na rika zingine na hivyo kupelekea wengi wao kudhohofisha nguvu kazi ya Taifa na mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
Takwmimu zinaonesha kuwa, watu milioni 35 wameshafariki dunia kutokana na maradhi yanayoambatana na virusi vya UKIMWI tangu ugonjwa huo ugundulike mwaka 1984 na Tanzania ina watu milioni 1.7 walio na VVU.