Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo Agosti 6, 2021 amewaongoza viongozi mbalimbali katika viwanja vya Karimjee kuaga mwili wa Marehemu Elias John Kwandikwa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na kujenga Taifa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akiongoza Viongozi mbalimbali na Wananchi  kuaga Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa  marehemu  Elias John Kwandikwa katika Viwanja vya Karimjee  Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akiifariji Familia ya aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa  marehemu Elias John Kwandikwa baada ya kuongoza Viongozi mbalimbali na Wananchi kuaga Mwili wa Hayati Kwandikwa katika Viwanja vya Karimjee  Jijini Dar es Salaam leo tarehe  06, Agosti 2021
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango na Mkewe Mama Mbonimpawe Mpango wakitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Marehemu Elias Kwandikwa katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam leo Agosti 6,2021.



Rais Samia -Kwandikwa alikuwa kiongozi mwadilifu
Chamuriho atoa maagizo haya kwa mtendaji mkuu mpya TANROADS