Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa amemkabidhi taarifa ya maandalizi ya Sensa ya watu na makazi Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan inayotarajiwa kufanyika mwezi Agosti, 2022

Dkt. Chuwa amesema Sensa ya mwaka 2022 itatumia teknolojia ya kisasa ya Kidijitali chini ya mfumo ulipo wa Serikali katika ngazi zote za Utawala kwa pande zote za Muungano.

Aidha, amesema Sensa ya majaribio itafanyika mwezi Agosti mwaka huu (2021) katika mikoa saba kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar.

Sensa ya Watu na Makazi ni zoezi la kitaifa linalofanyika kila baada ya miaka 10 ambapo Sensa ya mwisho kufanyika nchini ni mwaka 2012, hivyo Sensa ya mwaka 2022 itakuwa ni sensa ya Sita kufanyika nchini baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.

Fedha za tozo ya miamala ya simu hazitatumika kulipa mishahara -Dkt. Nchemba
Kamati ya uchaguzi TFF yaitwa Mahakamani