Katibu mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na wenye Ulemavu) Prof. Jamal Katundu amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maboresho aliyoyafanya katika vyuo vya watu wenye ulemavu.

Prof. Katundu ametoa pongezi hizo jijini Dodoma katika kongamano la kitaifa la Vijana na kusema kwa mwaka jana alitoa Bilioni 6.4 kwa ajili ya ukarabati wa vyuo hivyo.

“Mwaka jana zilitolewa Bilioni 6.4 kwaajili ya ukarabati wa vyuo hivyo na sasa tunaona vyupo vipo vizuri katika suala la ujenzi na vijana wetu wanaendelea kujipatia elimu katika mazingira mazuri”, amesema Prof. Katundu.

Aidha, ameongeza kuwa kwa jitihada hizo wanategemea vijana watakuwa na uwezo wa kuajiriwa wakiwa na ujuzi unao hitaji katika kupambania ajira nchini na kwamba wanatarajia ongezeko la ajira kuongezeka zaidi.

Hata hivyo, baadhi ya vijana waliohudhuria kongamano hilo walipata wasaa wa kuzungmza changamoto mbalimbali zinazowakabili, likiwemo suala la mitaji na mikopo ya kufanyia bishara.

Miquissone atengewa dozi maalum Simba SC
TCDC kuimarisha mifumo ya kisasa kidijitali