RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan ametimiza ahadi ya kumpatia mtaji wa biashara na fedha za kujikimu shilingi milioni 5,310,000, Bw.Yassin Said mwenye ulemavu wa ngozi aliemuandikia barua Rais akiomba kuwezeshwa kiuchumi baada ya kupitia masaibu katika maisha yake.

Akikabidhi fedha hizo kwa niaba ya Rais Samia, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amemsisitiza kijana Yassin kutumia fedha alizopatiwa kujiimarisha kiuchumi ili lengo la Rais kutoa fedha hizo liweze kutimia.

Kwa upande wake, Yassin Said amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa msaada aliopatiwa na kuahidi kuzitumia kwa lengo lililokusudiwa.

Serikali kuweka Mfumo kuwazuia wanyamapori uraiani
Serikali kuwekeza katika lishe kupambana na utapiamlo