Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameshiriki Ibada ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Mmliki wa Kampuni ya Montage ya uratibu wa matukio na Mdau wa Habari Marehemu Teddy Holo Mapunda.

Ibada hiyo imefanyika leo Mei 9, 2021 katika viwanja vya Kareem Jee, Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akitoa Heshima za mwisho kwenye Jeneza lenye mwili wa Marehemu Teddy Mapunda katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam leo tarehe 09 Mei, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha maombelezo kabla ya kuaga mwili wa Marehemu Teddy Mapunda katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam leo tarehe 09 Mei, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi wengine wakati wa shughuli za kumuaga Marehemu Teddy Mapunda katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam leo tarehe 09 Mei, 2021.
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Mei 10, 2021
Serikali yatangaza nafasi za ajira