Rais Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania ambao wanaishi maeneo yeye uwezo wa Muhimbili mazao ya chikichi na alizeti kuhamia kwenye kilimo hicho ilio kuikwamua nchi kutoka kwenye uhaba wa Mafuta.
Rais Samia amesema hayo leo wakati akihutubia wananchi alipokua uwanja wa CCM Ali Hassan Mwinyi katika kuhitimisha ziara yace ya siku tatu Mkoani Tabora.
Amesema wakulima, viongozi wa wizara husika pamoja na wadau wa kilimo washirikiane kutafuta maeneo ambayo ni makubwa yahusike na Kilimo hicho.
“Hatuwezi kuondoa uhaba wa mafuta ya kula nchini kama hatutafanya kilimo cha Alizeti na Michikichi katika maeneo makubwa, tukate maeneo makubwa ambayo hayatakuwa na matumizi sasa hivi yaende kwenye kilimo kikubwa na tutumie mbegu za kisasa,” amesema Rais Samia.
Ameongeza kuwa Nchi imeanza kuchukua hatua za kufanya kilimo kuwa cha maendeleo, “Tumeanza kuchukua hatua kukigeuza kilimo, ikiwemo kuanza kutoa ruzuku kwa Wakulima ambapo mwaka jana kwenye zao la Korosho tulitoa ruzuku ya Shilingi bilioni 51 na kwenye bajeti ya mwaka huu kuna ruzuku ya Shilingi bilioni 90 pia kwenye zao la Pamba mwaka huu imetengewa ruzuku ya Shilingi bilioni 56.”
Rais Samia amesem kuanzia mwaka mpya wa fedha 2022/2023, Serikali imeweka mkazo mkubwa kwenye masuala ya kilimo, uvuvi na ufugaji na fedha nyingi imewekwa kwa kuwa ni sekta zinazomgusa mwananchi moja kwa moja.
Aidha Rais Samia amesema kwenye zao la Tumbaku kuna ruzuku ya Shilingi bilioni 11.2 na riba katika sekta ya kilimo imeshuka mpaka asilimia 9 pia kumeanzishwa bima ya kilimo.
“Serikali tunaendelea kuweka mikakati ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji ambapo kwa mwaka mpya wa fedha tumeongeza Bajeti ya sekta ya umwagiliaji kutoka Shilingi bilioni 40 hadi Shilingi bilioni 361.” Ameongeza.
Rais Samia alikuwa ziarani Mkoani Tabora kwa siku tatu akikagua miradi ya maendeleo na leo amehitimisha ziara hiyo kwa kuhutubia wananchi.