Watanzania wametahadharishwa na wametakiwa kuchukua tahadhari zote dhidi ya mvua za vuli zinazotarajiwa kunyesha kwa wingi msimu huu.
Wito huo umetolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amewaomba Viongozi na Wananchi kuchukua tahadhari kwa lengo la kujiepusha na aina mbalimbali za maafa.
Amesema, “tunasali ili mvua hizi ziwe za kawaida ili zilete neema na baraka Nchini, lakini ikimpendeza Mungu zikawe nyingi basi zisituletee athari.”
Dkt. Samia ametoa rai hiyo wakati akipokelewa na mamia ya wakazi wa Mkoa wa Singida eneo la Sagara akiwa katika ziara ya kikazi ambapo pia akiwa Mkoani humo alifungua shule 302 zilizojengwa kwa mradi wa Boost na Sequip.