Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametaja idadi ya wagonjwa wa corona nchini, wanaotokana na wimbi la tatu la virusi hivyo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam alipokutana na wahariri wa vyombo vya habari, Rais Samia amesema kuwa kuna wagonjwa zaidi ya 100 wa corona ambao wamelazwa katika hospitali mbalimbali, wengi wakiwa katika hali mbaya wakipumua kwa msaada wa mitungi ya gesi.

“Nataka niwe mkweli, Tanzania tuna wagonjwa katika hili wimbi la tatu. Mpaka taarifa nilizozipata juzi, nadhani kuna wagonjwa kama 100 na…, kati yao si chini ya 70 wako kwenye matibabu ya gesi, wengine wako kwenye matibabu ya kawaida,” Rais Samia amesema.

Amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kwa kuzingatia ushauri unatolewa na watalaam wa tiba nchini, pamoja na kutumia njia anuai ambazo ni kwa ajili ya kupambana na ugonjwa huo.

Rais Samia amewaambia wahariri kuwa Tanzania imeruhusu chanjo dhidi ya corona kuingia nchini, na kwamba itakuwa hiari kwa kila Mtanzania kuchanja au la.

Rais Samia: Kuhusu Katiba Mpya, mikutano ya vyama vya siasa
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Juni 29, 2021