Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Wakuu wa Wilaya kwa kutengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mwanahamisi Athumani Munkunda na kumteua Mobhare Holmes Matingi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Mkurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa Rais Samia pia ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Abel Yeji Busalama na kumhamisha kituo Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini, Hashim Shaib Mgandilwa kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Aidha, Rais Samia pia amemteua James Wilbert Kaji, kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini akichukua nafasi ya Hashim Mgandilwa, aliyehamishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi

James Kaji, amewahi kuhudumu kama Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya kabla ya nafasi yake kutenguliwa Aprili 5, 2021.

Ibrahim Ajibu: Wachezaji wengi waoga Ligi Kuu
Dili la Declan Rice kukamilishwa juma hili