Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Nigeria, Olusegun Obasanjo.

Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, ambapo Rais Mstaafu Obasanjo ametoa salamu zake za rambirambi kwa Rais Samia kufuatia vifo vya waliokuwa Marais wa Tanzania ambao ni Mzee Benjamin Mkapa na Dkt. John Magufuli.

Aidha Rais Mstaafu Obasanjo amempongeza Rais Samia kwa kupokea kijiti cha kuwa Rais wa Tanzania na amemtakia heri katika majukumu yake.

Hata hivyo katika mazungumzo hayo Viongozi hao wamezungumzia hali ya usalama barani Afrika na umuhimu wa Wakuu wa nchi kujadiliana na kutafuta suluhisho la migogoro barani Afrika, inayosababisha vifo vya watu wasio na hatia hasa Wanawake na Watoto.

Sambamba na hayo Viongozi hao wamezungumzia masuala ya maendeleo hasa katika uchumi na kusisitiza umuhimu wa nchi za Afrika kuongeza ushirikiano na kuondoa vikwazo vya biashara na uwekezaji.

Katiba ya TFF, TOC haiwalindi viongozi - Gekul
Rais Samia atumbua vigogo TASAC, Posta