Katika kuadhimisha miaka 57 ya Muungano wa Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan ametoa msamaha kwa wafungwa 5,001 waliokuwa wakikabiliwa na adhabu ya vifungo mbalimbali.

Rais Samia amewataka wafungwa wote walioachiwa huru kutumia vema mafunzo waliyopata gerezani na waungane na Wananchi wenzao katika ujenzi wa Taifa, kuheshimu na kuzingatia sheria.

Miongoni mwa Wafungwa hao waliopewa msamaha na Rais leo, 1516 wameachiwa huru baada ya kupunguziwa robo ya adhabu na Wafungwa 3,485 wamepunguziwa robo ya adhabu badala ya punguzo la kawaida la theluthi moja na wataendelea kutumikia sehemu ya kifungo iliyobaki.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Aprili 27, 2021
Diamond awashauri Harmonize na Rayvanny, ‘watuige mimi na Ali Kiba’