Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amawaomba viongozi wa dini pamoja na machifu kusaidia kuirejesha jamii karibu na mungu ili kuondoa wimbi la mauaji ya raia ambalo linashamiri kote nchini.
Akizungumza katika maadhimisho ya jubilei ya miaka 25 ya Askofu Severine Niwemugizi katika viwanja vya Posta – Ngara Mjini, mkoani Kagera, Rais Samia amekiri uwepo wa vitendo vya mauaji na kujiua kwa raia katika maeneo mbalimbali nchini.
“Kumekuwa na Matukio mengi ya mauji na watu kujiua kwa kipindi hiki,” amesema nakuongeza kuwa Takwimu zinaonesha katika wilaya ya Ngara (mkoani Kagera) pekee mwaka 2020 kulikuwa na matukio 22 ya mauaji, Mwaka 2021 (21), Mwaka 2020 kulikua na matukio matatu ya watu kujiua na mwaka 2021 matukio mawili.
Rais Samia amesema serikali imekuwa ikiunda tume ndani ya jeshi la polisi kuchunguza sababu za mauaji. Hata hivyo taarifa za uchunguzi zimekuwa zikionesha chanzo kikiwa ni mapenzi, ugumu wa maisha, imani za kishirikina na mambo mengine.