Kampuni ya uzalishaji wa Vifaranga na Chakula cha Kuku, Silverlands imesema inaanzisha mpango mahususi utakaoishirikiana na Programu ya BBT Mifugo kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kuwawezesha vijana na akinamama katika sekta ya ufugaji, ili kukuza uchumi jumuishi na kupunguza mikopo kausha damu kwenye jamii.
Hayo yamebainishwa hii leo Agosti 2, 2023 jijini Arusha na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega wakati akizinduzia mtambo wa kuangua Vifaranga vya kuku katika hafla iliyofanyika.
Amesema, “mipango yetu kwa sasa, ni kuibadilisha tasnia kutoka kwenye ufugaji wa Kuku wa kimazoea kwenda kwenye ufugaji wa kisasa na wenye tija kwa wafugaji. Nawataarifu Watanzania wote kwamba Silverlands wako na BBT kwa upande wa ufugaji kuku. nawakaribisha na wawekezaji wengine wanofanya kazi hii ya kuku na wao kuungana na serikali.”
Hata hivyo, Waziri Ulega ameeleza kuwa BBT inafanya vizuri kwenye upande wa mazao, ufugaji wa ng’ombe na Samaki, na hivyo anawakaribisha wawekezaji waingie pia kwenye ufugaji wa kuku ambao unapendwa zaidi na vijana na kimanana wengi.