Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi na kuvunja Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania – TCRA.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa, Rais Samia amemteua Balozi James Gilawa Bwana, kuwa Balozi wa Tanzania nchini Afrika kusini akichukua nafasi ya Balozi Meja Jenerali Gaudence Salim Milanzi ambaye amestaafu.

Aidha, amemteua Balozi Said Hussein Massoro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, akichukua nafasi ya Balozi Said Shaib Mussa ambaye aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki.

Taarifa hiyo pia inaonesha Rais Samia amemteua Kaimu Abdi Mkeyenge kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa – NIC, ambapo kabla ya uteuzi huo Mkeyenge alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Nchini – TASAC, akichukua nafasi ya Dkt. Elirehema Doriye ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Tumieni busara kuwaonya Viongozi wa Serikali - Mlao
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Novemba 9, 2023