Wafanyabishara wa Soko la Wamachinga lililopo Old Airport Mbeya, wameipongeza Serikali kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dkt Tulia Ackson kwa Jitihada kubwa za kuboresha Miundombinu ya Soko hilo.
Wakizungumza kwenye Mkutano wa hadhara wa kusikiliza na kutatua kero za Wafanyabishara wa Soko hilo wameonesha kuguswa na Jitihada za Serikali kuboresha Miundombinu ya Soko hilo hali itakayo wavutia Kufanya biashara zao bila kikwazo.
Aidha, Wafanyabishara hao pia wamesisitiza kuwa Serikali iboreshe zaidi Barabara zinazoingia Sokoni hapo ili kurahisisha huduma na usafiri.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, John Nchimbi amesema utaratibu wa Ujenzi wa Barabara unaendelea huku hatua za awali zikifanywa Ili kuanza Utaratibu wa Ujenzi wa barabara inayotoka Kabwe Kuelekea OldAirport.
Akitolea Ufafanuzi wa hayo Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa amesema Serikali ya awamu ya Sita itaendelea Kushirikiana na Wafanyabishara wadogo Machinga kwa kuwaboreshea mazingira ya kifanyia biashara zao.