Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasili nchini Uganda, kwa ziara ya kikazi ya siku moja kwa mwaliko wa Rais Yoweri Museveni wa nchi hiyo.

Akiwa nchini Uganda pamoja na mambo mengine, Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na mwenyeji wake Rais Museveni, watahudhuria hafla na kushuhudia utiaji saini wa mkataba kati ya Serikali ya Uganda na Kampuni ya Mafuta Ghafi ya Afrika Mashariki (EACOP) juu ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la kutoka Hoima nchini Uganda kwenda Tanga nchini Tanzania.

Rais Samia aliondoka nchini kupelekea nchini Uganda mapema asubuhi leo Aprili 11, 2021 kwa ziara hiyo ya siku moja na kushuhudia utiliaji saini wa mkataba huo.

Mwanamfalme Philip kuzikwa terehe 17
Faida za vitunguu swaumu kwa wanaume