Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewatakia Waumini wa dini ya Kiislamu wote mfungo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Rais Samia Suluhu Hassan, amewaomba Waislamu kuiombea nchi amani, upendo, mshikamano na utulivu ili kujenga mazingira bora zaidi kwa maendeleo na ustawi wa jamii.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Rais Samia ameamdika “Nawatakia Waislamu wote mfungo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Tukiwa katika kipindi hiki cha toba tusisahau kuiombea nchi yetu amani, upendo, mshikamano na utulivu ili kujenga mazingira bora zaidi kwa maendeleo na ustawi wa jamii. Ramadhan Kareem wa Swaum Maqbul.”

Ibada ya funga itaanza kesho Aprili 14, 2021 kwa Waislamu, ikiwa ni moja ya nguzo za Uislamu.

Ndugai amtupia kijembe Mbowe, 'alikuwa mzururaji'
Mtoto wa darasa la tatu afariki akiigiza watu wanavyojinyonga