Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt, Samia Suluhu Hassan leo Oktoba 15, 2023 amefungua Shule ya Msingi Imbele na shule ya Sekondari Mwanamwema kwa Niaba ya Shule Mpya 302 Zilizojengwa Nchi Nzima kupitia program ya BOOST na SEQUIP na kutoa wito kwa Wazazi kuwapeleka wototo Shule.

Rais Dkt, Samia amezindua Shule hizo wakati wa Ziara ya Kikazi Mkoani Singida ambapo pia amesema Serikali imedhamiria kuboresha elimu na kumuandaa mtoto kuanzia awali mpaka elimu ya juu.

Katika hatua nyingine, Dkt. Samia amewataka Wananchi wa Mkoa wa Singida kuchukua tahadhari ya Mvua za Vuli  zinazotarajiwa kuanza kunyesha Nchini.

Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na Wananchi wa Sagara Mkoani Singida, alipowasili hii leo akitokea Manyara ambapo atakuwa na ziara ya kikazi mkoani humo.

Picha: Uzinduzi Shule 302 zilizojengwa kwa mradi wa BOOST, SEQUIP
Umeme Vijijini: Bado Vijiji sita - Kapinga