Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Baraza la Eid ambalo kitaifa litafanyika mkoani Dar es Salaam.

Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Aboubakar Zuber ametoa taarifa hiyo wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya watu wenye ulemavu, wajane na watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Sheikh Mkuu amewataka waumuni wa Dini ya Kiislamu na wasio Waislamu kujitokeza kwa wingi kuhudhuria Baraza la Eid ambalo kwa mwaka huu litahutubiwa na Rais Samia Suluhu Hassan na litafanyika jijini Dar es Salaam.

Aidha, Sheikh Zubeir amewataka waumini wote wa dini ya Kiislamu kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu katika mwezi huu wa Ramadhani na wakati wote ili aendelee kujalia heri nchi ya Tanzania.

Salva Kiir atangaza Bunge jipya
Tatueni kero za jamii- Naibu Waziri wa Afya