Rais wa Uganda Yoweri Museveni anatarajia kuwasili wilayani Chato Novemba 29, 2021 kwaajili ya kumkabidhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan shule ya msingi Museveni ya mchepuo wa Kiingereza iliyojengwa na serikali ya Uganda.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Rosemary Senyamule ameeleza kuwa shule hiyo ni shule ya msingi mbayo itakuwa inatumia lugha ya kiingereza.
”Shule hiyo ni shule ya msingi ambayo itakuwa inatumia lugha ya kiingereza na inategemea kupokea wanafunzi kuanzia shule ya awali na kwenda darasa la kwanza mpaka darasa la sabaa mpaka sasa ametujengea madarasa 20 kati ya hayo madarasa 17 ni madarasa kwaajili ya darasa la kwanza mpaka la saba na madarasa matatu ni kwaajili ya mafunzo ya awali”amesema RC Senyamule
Aidha ametoa wito kwa wazazi ambapo amesema kuweza kujitokeza kwa wingi kupeleka watoto katika shule hiyo ambayo inamilikiwa na serikali na inatumia lugha ya kiingereza kufundishia.
”Wananchi wa Geita na watanzania kwa ujumla kujitokeza kuleta watoto kwenye shule hiyo tunajua kuwa wazazi wengi huwa wanatumia gharama kubwa kupeleka watoto kwenye shule za lugha ya kiingereza lakini shule hii kwa sababu ya kumilikiwa na serikali na walimu wapo gharama yake huenda ikawa chini kidogo kuliko shule zingine” amesema RC Senyamule