Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kesho Mei 7, 2021 anatarajia kuzungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam katika mkutano utakaofanyika ukumbi wa Mlimani City na kuhusisha wazee takribani 900.

Hayo yameelezwa leo Mei 6, 2021 na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge ambapo amesema kuwa kulikuwa na utaratibu maalum wa kuwapata wazee hao na kwamba wengine wanapaswa kufuatilia mkutano huo kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

“Tunamshukuru Rais kwa kuchagua Mkoa huu kwa sababu angenda Mkoa wowote lakini amechagua Dar es Salaam. Ninaamini kuongea na wazee hao atakuwa ameongea na wazee wa Tanzania nzima,” amesema Kunenge.

Aidha, Kunenge amesisitiza kwa wazee wote waliopata mwaliko huo kuhudhuria bila kukosa na kueleza kuwa kuna utaratibu maalum wa magari ambao umeandaliwa wa jinsi ya kuwafikisha wahusika hao.

Wizara ya maji yawasilisha bajeti ya bilioni 680
Bunge lakosa maswali kwa Waziri Mkuu