Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuhutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Taifa, Alhamisi April 22, 2021.

Taarifa hiyo imetolewa na Spika wa Bunge, Job Ndugai leo Aprili 19, 2021 Bungeni jini Dodoma ambapo amesema, “Tarehe 22, siku ya Alhamisi Mheshimwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan atakuja hapa Bungeni, kwa ajili ya kulihutubia Bunge, na kwa maana hiyo kuwahutubia Wananchi wa Tanzania wote kupitia Bunge.”

Spika Ndugai ameeleza kuwa baada ya Rais Samia kulihutubia Bunge, kutakuwa na futari ya pamoja iliyoandaliwa na Rais mwenyewe kwa Wabunge, Watumishi wa Bunge pamoja na Viongozi wote watakaikuwa wamealikwa siku hiyo.

Spika ametoa wito kwa Wabunge wote kuwepo Bungeni siku hiyo wakati Rais atapokuwa anahutubia.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Samia kuhutubia Bunge kama Rais, tangu kuapishwa kwake kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Machi 19, 2021 baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Fiston kuondoka Young Africans
Gomes: Young Africans wasahau kuhusu ubingwa.

Comments

comments